Kagame tayari anadai kuwa mshindi katika uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika tarahe nne mwezi ujao.

Rais wa Rwanda Paul Kagame tayari anadai kuwa mshindi katika uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika tarahe nne mwezi ujao.

Kagame jana aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa kwanza wa kuanza rasmi kwa kampeini nchini humo kuwa matokeo ya uchaguzi tayari yalijulikana mnamo mwaka 2015 wakati zaidi ya Wanyarwanda milioni nne waliposhiriki katika kura ya maoni ili bunge kuifanyia katiba mageuzi ya kumruhusu kugombea muhula mwingine madarakani.

Kagame amesema wapinzani wake hawawezi kubadilisha mapenzi ya wananchi kuwa yeye ndiye chaguo pekee kwa warandwa.

Rais huyo wa Rwanda amekuwa madarakani tangu kukamilika kwa mauaji ya halaiki yaliyoikumba nchi hiyo mwaka 1994,Licha ya kuwa anasifiwa kwa kuleta uthabiti katika taifa hilo la takriban watu milioni 12.

Aidha anashutumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia mkono wa chuma kuliongoza taifa na kuwakandamiza wapinzani nchini humo.

Wagombea wengine wa urais ni Frank Habineza wa chama cha Democratic Green na mgombea huru Philippe Mpayimana.

 

Exit mobile version