Jana miili ya watoto wawili imeopolewa katika shimo lililodaiwa kuwa ni shimo la choo eneo la Mji Mpya, katika Mtaa wa Olkerian jijini Arusha.
Tukio hilo lilithibitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo uliopo Kata ya Olasiti Daudi Safari, ambapo ameeleza kutokea kwa tukio hilo la kukutwa miili ya watoto ambayo haijatambuliwa bado.
Kazi ya uopoaji miili hiyo ilitekelezwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
Kufuatia tukio hilo leo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amezungumza na wanahabari na kueleza yafuatayo.
