Kamati ya Maadili,Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania yawasilisha Bungeni taarifa za matukio mbali mbali ambazo imezifanyia kazi.

In Kitaifa

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.

Aidha, Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.

Pia Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee  kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.

Hata hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo  baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .

Katika hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBA 7, 2023

Manchester United na Newcastle United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 20, ambaye mkataba wake unamalizika Juni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu