KAMISHNA WA TUME HURU YA UCHAGUZI NA MIPAKA (IEBC) AJIUZULU.

In Kimataifa


Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Dk Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu nafasi yake katika tume hiyo.

Dk Akombe ametuma taarifa ya kujiuzulu akiwa mjini New York nchini Marekani anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kaziUmoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.

Katika taarifa yake, Akombe amesema kwamba uchaguzi wamarudio wa uraisi uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu haujafikia vigezo vya kuwa uchaguzi huru na wa haki.

Akombe anajiondoa kwenye tume hiyo ya IEBC ikiwa imebakiwiki moja uchaguzi wa urais kurudiwa kutokana na matokeo ya awali kufutwa na mahakama kuu na kuamuru uchaguzi mpyaufanyike.

Agosti Akombe alizuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa JKIA akielekea nchini Marekani.

Dk Roselyn Akombe Kwamboka alizaliwa 1976 katika kaunti ya Nyamira , na kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi kabla yakuelekea nchini Marekani kwa masomo zaidi.

Ana shahada ya uzamifu katika masuala ya sayansi na kimataifa mbali na shahada nyengine kama hiyo katika somo hilo kutoka chuo kikuu cha Rutgers .

Hadi uteuzi wake katika tume hiyo alifanya kazi kama katibu katika Umoja wa Mataifa mjini New York, wadhfa ambao anasema ulimwezesha kuwa na uzoefu katika maswala hayo na uwezo wake mkuu amesema mbele ya kamati ya bunge nchini Kenya, ni kutatua migogoro na kwamba ameishi ng’ambo kwa takriban miaka 15,hatua iliomwezesha kuelewa zaidi mahitaji ya watu wanaoishi ughaibuni wakati wa uchaguzi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu