Kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu yazinduliwa”.

In Kitaifa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, leo Mjini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.

“Historia ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali,” ameeleza Jafo.

Aidha amesema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini

“TAMISEMI kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko,” amefafanua Jafo.

Hata hivyo, Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na Halmashauri kuwatumia ipasavyo Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ugani ili kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga majengo maalumu kwa ajili ya uendelezaji viwanda katika Ofisi zote za SIDO Mikoani.

Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa Kauli Mbiu ya Mkoa wetu viwanda vyetu itapunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu