Kampuni ya Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (Udart) imekiri kufanya makosa.

Kampuni ya Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (Udart) imekiri kufanya makosa kwa kutofikisha taarifa vituoni kwa wateja wanaotumia usafiri huo kuhusu matatizo yanayotokea kwenye mabasi hayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema hayo baada ya mabasi hayo kugongana eneo la Shekilango na kusababisha barabara kutopitika.

Amesema kufuatia ajali ilitakiwa abiria wapatiwe taarifa wakiwa kwenye vituo vyao, lakini haikuwa hivyo na badala yake wakawa wanashindwa kujua nini kinaendelea.

Deus amesema kilichojitokeza ni tatizo la kibinadamu, hivyo amewataka watu wawe waelewa.

Exit mobile version