KARIM BENZEMA ASHINDA BALLON D’Or KWA MARA YA KWANZA

In Kimataifa, Michezo
Karim Benzema: Mshambulizi wa Real Madrid ashinda Ballon d'Or kwa wanaume kwa mara ya kwanza
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Club ya realmadrid ya Hispania Karim Benzema ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia(Ballon D’or), Tuzo hizo zimetolewa nchini Ufaransa.

Benzema alifunga mabao 44 katika mechi 46 msimu uliopita akiwa na Real Madrid, walioshinda LaLiga na Ligi ya Mabingwa; Sadio Mane alimaliza katika nafasi ya pili huku Kevin De Bruyne akiwa wa tatu; Kiungo wa Barcelona Gavi alipewa Kombe la Kopa kama mchezaji bora chipukizi wa mwaka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga mabao 44 katika mechi 46 msimu uliopita Real ikishinda Ligi ya Mabingwa, taji lingine la LaLiga pamoja na Kombe la Super Cup la Uhispania na Uropa.

"Inanifanya nijivunie sana," alisema Benzema. "Kazi zote nilizofanya, sikukata tamaa. Ilikuwa ndoto ya utotoni kama watoto wote [wanayo]. Nilikuwa na motisha mbili katika maisha yangu - Zidane na Ronaldo. Siku zote nimekuwa na ndoto hii akilini mwangu kwamba chochote kinawezekana".

"Kulikuwa na kipindi kigumu ambapo sikuwa katika timu ya Ufaransa, lakini sikuacha kufanya kazi kwa bidii wala kukata tamaa. Siku zote niliweka kichwa changu, nikizingatia kucheza mpira na ninajivunia safari yangu ya hapa. t rahisi, ulikuwa wakati mgumu. Ilikuwa ngumu kwa familia yangu pia. Kuwa hapa leo, kwa mara ya kwanza kwangu, nina furaha na kufurahishwa na kazi yangu na ninaendelea."

"Nataka kuwashukuru wachezaji wenzangu, iwe ni Real Madrid au timu ya taifa. Kocha wangu, asante pia. Rais wa Real Madrid pia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu