Kasi ya utendaji kazi ya DAWASCO yamridhisha Prof.Kitila Mkumbo.

In Kitaifa

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa anaridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa DAWASCO, katika kusimamia miradi mbalimbali ya maji.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayosimamiwa na DAWASCO,ambapo amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kutoa huduma za maji kwa wakazi zaidi ya laki mbili, kwa mikoa ya Pwani na Dar es salaam.

Hata hivyo, Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu, Mradi wa uchimbaji  Visima virefu Kimbiji na Mpera, Chanzo cha maji Wami unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.

 

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu