Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Athanas Rugambwa
Miaka 62 mkazi wa Muganza wilayani Chato mkoani Geita,kwa
tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka nane mwanafunzi wa
darasa la tatu shule ya msingi Katema.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Septemba
15, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani humo Henry Mwaibambe,
amesema mtuhumiwa ni Katekista na alikua akimfundisha mtoto
huyo masomo ya dini.
Mwaibambe amesema mtuhumiwa huyo alimvizia mtoto akiwa
kwenye mafundisho ya dini kanisani na kumuita ofisini kwake
kisha kumbaka.
