Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Sharif Hamad Seif amemlaumu msajili wa vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kuunda bodi ya wadhamini feki wa chama hicho.
Ameyasema hayo jana Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa wamefanya hivyo ili kuweza kumsaidia Prof. Lipumba ambaye alijiuzuru kwa matakwa yake mwenyewe.
Amesema kuwa RITA imepata shinikizo kusajili wajumbe feki wa Bodi ya wadhamini wa CUF kwa kutumia majina yaliyowasilishwa na Prof. Ibrahimu Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Uongozi wa la Taifa kupitia kikao chake kilichofanyika makao makuu ya chama Zanzibar.
Hata hivyo, ameongeza kuwa hujuma iliyofanywa na RITA kwa kushirikiana na Msajili wa vyama vya Siasa nchini na Prof. Lipumba haiwezi kusaidia chochote katika kukiimarisha chama hicho
