Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kuitega amesema serikali ina wajibu wa kuanza kusaidia kituo cha Kuhudumia watoto cha SOS,ambacho kilikuwa kinahudumiwa na wafadhali kutoka nje ya nchi.
Akizungumza wakati alipotembelea taasisi inayohudumia watoto yatima ijulikanayo kama SOS children iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha katibu huyo, amesema serikali ina Jukumu la kutoa ushirikiano ili kuweza kuendeleza miradi mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi
Kuitega amesema kuwa serikali itaanza kwa kutoa wataalamu watakao toa huduma kituoni hapo kama vile walimu ili kuhakikisha kuwa wanapunguza baadhi ya changamoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Fransis Msolo amesema kituo hicho kilikuwa chini ya wafadhili ,ambao kwa sasa wanajitoa hivyo ipo haja ya serikali kupandisha hadhi kituo hicho ili kiweze kutoa huduma ndani ya Jamii.
Halikadhalika taasisi hiyo imeweza kutunza watoto Elfu moja 1000 ambapo wengine amefika hadi elimu ya Juu ya Vyuo Vikuu na kuweza kujiendeleza Kimaisha.
