Kauli ya mpango kwa wanorubuni wanafunzi.

In Kitaifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Philip Mpango,ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha
wanasimamia vema watoto wao kupata elimu kwa mustakbali
wa Maisha yao, na kuwa na uhakika wa wataalamu mbalimbali
wa baadae kwa manufaa ya taifa.


Makamu wa Rais amesema hayo aliposhiriki hafla ya kukabidhi
madarasa matatu,ofisi mbili na samani katika shule ya Muyama
iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma alipopata elimu yake
ya msingi mwaka 1968-1970,madarasa ambayo yamekarabatiwa
na Benki ya Biashara Tanzania TCB.


Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameahidi kuanzisha
tuzo maalum zitakazoenda na zawadi kwa wanaofanya vizuri
katika shule hiyo,ili kuongeza ushindani na ari kwa walimu na
wanafunzi wa shule hiyo.

Akiwa mkoani humo pia amezindua Hoteli ya Kisasa ya Bwami
Dubai ambayo imegharimu bilioni 1.6 iliyojengwa na mzawa wa
Kigoma Evance Chocha katika Wilaya ya Kasulu mkoani humo.


Amesema serikali inatambua mchango wa wazawa na wageni
katika kuchochea maendeleo ya mkoa wa Kigoma na Taifa kwa
ujumla,na kutoa wito kwa watanzania wote hususani wa mkoa
wa Kigoma kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika
mkoa huo ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu