Kwa mara ya kwanza tarehe 12 Disemba sherehe za maadhimisho ya Kenya kulijipatia uhuru, zimefanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani.
Maadhimisho hayo ya 54 tangu Kenya ilipojipatia Uhuru wake mwaka 1963, yameongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Sherehe hizo zilikuwa na utumbuizaji wa kila aina, zikiwemo nyimbo za kitamaduni na dini, michezo ya kuigiza, mchezo wa kwata, na maonyesho ya ndege za kijeshi, pamoja na gwaride maalum ya vikosi vyote vya usalama.
Antenna tumeinasa sehemu ya hotuba ya Rais Uhuru Kenyata, aliyoitoa mapema leo katika sherehe hizo
