Kenya imeandaa mkakati wa usalama, ambao utatumika wakati wa kampeni na uchaguzi.Mkakati huo utajumuisha maafisa laki 1 na elfu 80, watakaopata mafunzo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Agosti 8.
Imeelezwa kuwa kupitia mpango huo, utawawezesha Wakenya kushiriki katika uchaguzi, katika njia inayodumisha umoja wa nchi.
Maafisa watakuwepo kulinda usalama, kuzuia vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani au visa vyovyote vya kuzua vurugu.
