Jana Rais Uhuru Kenyatta amekutana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo IEBC, huku uchaguzi wa marudio ambao umekumbwa na utata ukiendelea kukaribia.
Mwenyekiti huyo wa tume alikuwa amekutana na mgombea wa upinzani Bw Raila Odinga Ijumaa iliyopita.
Taarifa kutoka ikulu imesema Rais Kenyatta amemwambia mwenyekiti huyo kwamba, yuko tayari kwa uchaguzi huo na hana masharti yoyote kwa tume hiyo.
Wakati Kenyata akisisitiza uchaguzi huo upo, upande wa NASA, umesimamia msimamo wao kwa kusema kuwa hakuna uchaguuzi utakaofanyika.
