Kenyatta aapishwa kutekeleza majukumu ya urais.

Msajili wa Mahakama Anne Amadi, anamlisha sasa kiapo cha kutekeleza majukumu ya afisi ya rais.

Rais Kenyatta: “Nitatekeleza majukumu yangu, na wajibu wangu katika afisi ya rais wa Kenya, na kwamba nitatenda haki kwa wote kwa mujibu wa katiba hii kama ilivyo kwenye sheria, na sheria za Kenya bila woga, mapendeleo au ubaguzi au nia mbaya. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie.”

Baadaye, ametia saini viapo vyote viwili, kisha cheti cha kuapishwa, kuthibitisha kwamba sherehe ya leo imefanyika.

Jaji Mkuu David Maraga pia ataweka saini yake kwenye stakabadhi zote tatu (vipao viwili) na cheti cha kuapishwa kwa Rais.

Exit mobile version