Rais Uhuru Kenyatta ametetea hatua yake ya kuikosoa mahakama ya juu na jaji mkuu David Maraga, kwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais akisema ni haki yake kufanya hivyo.
Akizungumza katika kampeni za chama cha Jubilee eneo la Kajiado siku ya jana, Kenyatta amesisitiza madai yake kwamba mahakama hiyo ya juu ilipuuzilia mbali haki ya wananchi ili kumfurahisha mtu mmoja, aliyemtaja kuwa mpinzani wake Raila Odinga.
Amesema licha ya kuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo, anajua kwamba alishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya kura milioni 1.4.
Licha ya uamuzi huo Rais Kenyatta amesema kuwa ana imani atashinda tena uchaguzi huo wa marudio.
Insert 3-Kenyata
Kwa upande mwingine baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kutangaza kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi huo mpaka Tume ya Uchaguzi ifanyiwe mabadiliko.
Sasa habari mpya ni kuwa Tume hiyo imetangaza kundi la watu sita ambalo litasimamia uchaguzi huo.
Walioteuliwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba, Naibu wake Betty Nyabuto, Mkurugenzi wa Usajili wa wapiga kura pamoja na Mkuu wa Operesheni za Uchaguzi Immaculate Kasait, Naibu wake Mwaura Kamwati, Mkuu wa Operesheni za Tume na Mkuu wa Teknolojia James Muhati.
