Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita.
Hiyo ni asilimia 38.84.
