Kenyatta na Ruto wafunga sherehe kwa maombi.

Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wamekamilisha sherehe za leo uwanja wa Kasarani kwa maombi, Bw Kenyatta ameongoza kwa Kiingereza na Bw Ruto kwa Kiswahili.

Baadaye, wimbo wa Jumuiya ya EAC umechezwa na kisha wimbo wa taifa la Kenya kuhitimisha sherehe za leo.

Wageni wameanza kuondoka uwanjani, wakianza na viongozi wa nchi.

Exit mobile version