Hospitali ya Kagondo wilayani Muleba mkoani Kagera, imepata msaada wa visima vya maji kutoka Rotary Club ya Bukoba kwa kushirikiana na Rotary Club ya America, kwa ajili ya kupunguza changamoto ya maji inayosababisha huduma nyingine kutotekelezeka.
Akiongea kwa niaba ya Rais wa Rotary Club ya America, Rais wa Rotary Club ya Bukoba Dr Eunice Ntangeki, amesema kikundi chao kwa kushirikiana na wenzao wa America, waliomba msaada kwa wafadhili na kufanikiwa kupata Milioni 220 kwa ajili ya ujenzi wa Visima 13 vya kuvunia maji ya mvua, ambavyo vitakuwa na ujazo wa Lita 650,000.
Baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika mradi huo Mkuu wa Wilaya Muleba Mhandisi Richard Luyango, amewasihi wananachi ambao watanufaika na mradi huo, kuhakikisha wanautunza vizuri mara utakapoanza kazi, ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kumaliza changamoto zao