Kero za Muungano zapatiwa ufumbuzi.

In Kitaifa

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Luhaga Mpina, amesema Kero za Muungano, ambazo zimekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi zimepatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa.

Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja mbali mbali kutoka kwa wabunge.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2007 hoja 15 zilizowasilishwa kutafutiwa ufumbuzi kati ya hizo hoja 11 ,zimepatiwa ufumbuzi.

Aidha, ametaja kero hizo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Tume za Haki za Binadamu na utawala Bora, Uvuvi kwenye ukanda wa bahari Kuu, ushiriki wa Zanzibar kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, amezitaja kero zingine zilizopatiwa ufumbuzi ni ushiriki wa Zanzibar na Kampuni za Kimataifa, suala la ajira kwa raia wa Zanzibar, utafutaji na uchimbaji  wa mafuta na gesi asilia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu