Muongoza mashitaka wa jimbo ka Georgia Fani Willis Jumatano ametangaza tarehe ya kusikilizwa kwa kesi ya kuingilia uchaguzi wa 2020 dhidi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump pamoja na watu wengine 18.

Tarehe hiyo umetangazwa kuwa Machi 4 mwaka ujao, suala linaloongeza vizingiti kwenye kalenda ya Trump, wakati akijiandaa kuwania tena urais kwenye uchaguzi wa 2024. Jaji wa mahakama ya juu ya Kaunti ya Fullton Scott McAfee amechaguliwa miongoni mwa majaji wengine kusikiliza kesi hiyo kwenye mji mkuu wa kusini mwa Georgia wa Atlanta.
Hata hivyo mawakili wa Trump wanatarajiwa kuomba mahakama isogeze tarehe ya kusikilizwa na ikiwezekana hadi baada ya uchaguzi kufanyika Novemba mwakani. Iwapo Jaji McFee atakubaliana na tarehe iliyotolewa na kiongozi wa mashitaka ya Machi 4, basi ina maana kwamba itaanza siku moja kabla ya siku inayojulikana kama Super Tuesday, ambapo majimbo 14 hufanya uchaguzi wa kuteuwa wagombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu.