Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi ya utakatishaji fedha ya USD 300,000, inayowakabili Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange, hadi November 10 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Wakili wa Serikali Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu Victoria Nongwa kuwa, kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, pia ameeleza uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea na jalada la kesi bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi November 10 2017, na watuhumiwa kurudishwa rumande.
Evans Elieza Aveva na makamu wake Geofrey, wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
