Kesi ya washtumiwa wa mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa ilisikilizwa tena siku ya Jumatatu Julai 17. Mashahidi kadhaa muhimu waliotarajiwa kufika kusikilizwa katika mahakama ya kijeshi ya Kananga hawakufika.
Miongoni mwao, afisa iliekua akisimamia operesheni katika eneo ambapo wataalam walikutwa waliuawa.
Meja Mbuara Issa alihamishiwa Tshikapa. Pia hakuna taarifa kuhusu kiongozi alietajwa na washtumiwa wakuu, aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wanaodaiwa kushirikiana na na jeshi la DRC (FARDC).
Jean Bosco Mukanda ni shahidi mkuu kwa upande wa jeshi la DR Congo, Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na waandishi wa habari na Alikua mtu wa kwanza kurusha hewani habari za mauaji ya wataalam hao Michael Sharp na Zaida Catalan na alishtumu makundi ya wanamgambo wa eneo hilo kuwa ndio walihusika na mauaji ya wataalam hao.
Jean Bosco Mukanda alisema kuwa makundi ya wanamgambo ya Moyo-Musuila na Mulumba-Muteba yalihusika na mauaji ya wataalam wa Umoja wa Mataifa.
Taarifa za Bw Mukanda zinakwenda sambamba na zile zilizorushwa na radio ya Mbunge Clément Kanku, kiongozi wa zamani wa wanamgambo aliyebadili sura na kuwa mpashaji habari katika jeshi la DR Congo amesema kuwa laiona tukio zima.
Jean Bosco Mukanda ni mmoja wa watu waliosaidia kugunduliwa kwa miili ya wataalam hao wawili
