WADAU mbalimbali wa Maendeleo wamekutana katika Mkutano wa Maendeleo endelevu kwa viongozi wa Majiji kwa nchi za Afrika Nchini Belgium ,ambapo Tanzania imewakilishwa na Jiji la Arusha chini ya Mkurugenzi Athumani Kihamia na ofisi ya Jumuiya ya Ulaya Tanzania chini ya Afisa utekelezaji Anna Constantin kutoka Italy
Akizungumza na redio 5 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athman Kihamia amesema lengo la Mkutano huo ni kuziwezesha Serikali za Mitaa katika Maendeleo, hasa kilimo cha Mazao ya chakula.
Kihamia amesema mazao Mengi yamekuwa yakikosa namna bora ya uhifadhi haswa mazao ya Chakula hivyo kupitia Mkutano huo utawawezesha kutambua namna bora ya Utunzaji ili yapate soko yakiwa yamechakatwa ili kuleta tija zaidi.
Aidha amesema kuwa nchi ya Tanzania inapendeza sana kwa kuwa,na Sera nzuri na bora iliyopo Ya Viwanda hasa vya Wakulima Wadogo.
Mkutano huo umeshirikisha mataifa 43 kutoka barani Afrika vikiwemo Vyuo vikuu mbalimbali vya kilimo sayansi na teknolojia vya Madrid,Palacky,Hague,Toulouse Capitole, Antwelp na taasisi na mashirika mbalimbali ya maendeleo kama UNDP,EEAS, Kamisheni ya ulaya, wabunge wa jumuiya ya ulaya.
