Kijana mdogo ameuawa nchini Venezuela katika siku nyingine ya maandamano dhidi ya Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro, maandamano ambayo kwa sasa yanazorotesha uchumi wa taifa hilo.

Kijana mdogo ameuawa nchini Venezuela katika siku nyingine ya maandamano dhidi ya Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro, maandamano ambayo kwa sasa yanazorotesha uchumi wa taifa hilo.

Kijana mwenye umri wa miaka 17, Luis Alviarez alipigwa risasi kifuani katika maandamano ya upinzani kwenye mji wa Guasimo, Mashariki mwa nchi hiyo.

Wito umetolewa wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mazingira ya mauaji hayo.

Kiongozi wa wanafunzi mwenye umri wa miaka 22 Wilmer Arevalo naye yu mahututi baada ya kupigwa risasi kichwani kwenye maandamano mengine.

Pia kwenye jimbo la Tachira, wanaharakati wapinzani wa shirika la Foro penal wamesema zaidi ya watu 40 walikamatwa siku ya jumatatu .

Takriban watu 40 wameuawa tangu maandamano kuanza nchini humo majuma saba yaliyopita.

Exit mobile version