Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Kingunge Ngombale Mwiru, amewashangaa wanaoeneza taarifa kuwa yu mgonjwa na amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Leo akiwa nyumbani kwake Makumbusho jijini Dar es Salaam amesema yuko vizuri na hana tatizo lolote.
Amesema anaendelea kudunda kama kawaida, na kwamba leo asubuhi alifanya mazoezi ya kutembea kwa saa moja ili kuuweka sawa mwili wake.
Kingunge ameshauri kupuuzwa kwa taarifa hizo za mitandaoni, zinazosambazwa kueleza kuwa yu mgonjwa.
Tangu jana Alhamisi Novemba 9,2017 kwenye mitandao ya kijamii imesambazwa picha ikimuonyesha Kingunge akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akijuliwa hali na Rais mstaafu Jakaya Kikwete na mkewe Salma.
