Kiongozi wa zamani wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia Mukhtar Abu Mansur, amejiondoa kutoka kwenye kundi la wapiganaji hao na kujiunga na serikali ya Somalia.
Afisa wa jeshi la Somalia Kanali Nur Mohamed amesema kuwa, Mansur na walinzi wake 7 kwa sasa wako mjini Hudur, pamoja na maafisa wa serikali.
Kujitenga kwa Mansur na Al-Shabaab, kunajiri miezi miwili tangu Marekani kuondoa kima cha dola milioni 5 juu yake, kama zawadi kwa yeyote ambaye angewezesha kukamatwa kwake.
Mansur ambaye alikuwa naibu mkuu mtendaji wa Al-Shabaab, ndiye kiongozi wa ngazi ya juu kuwahi kuliacha kundi hilo.
