Jumanne, alikuwa amemwambia mkuu wa majeshi Jen Constantino Chiwenga anafaa “kusalia kwenye kambi za jeshi”.
Alisema wanachama wake hawatakubali wanajeshi wakiuke katiba na kwamba yeye na wafuasi wake walikuwa tayari kufariki wakimtetea Mugabe.
Lakini usiku wa kuamkia leo, alisoma taarifa kwenye runinga ya taifa ZBC, akisema kwamba alikuwa amekosea.
“Tangu wakati huo nimetafakari na kutambua binafsi kwamba nilikosea, pamoja na wakuu wenzangu kwa kudunisha afisi yako yenye heshima.”
“Sisi bado ni wadogo na hufanya makossa na tumejifunza mengi kutokana na makosa haya.”