Kipigo cha mabao 8-2 kinawafikirisha mastaa wengi wa Barcelona kusepa

Luis Suarez, staa wa Klabu ya Barcelona ni miongoni mwa
nyota wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kusepa ndani ya
klabu hiyo msimu ujao baada ya kupoteza kwa kichapo kikubwa
cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich.

Barcelona ilipokea kichapo hicho kwenye mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali na kushuhudia Bayern
Munich ikitinga hatua ya nusu fainali ambapo leo itacheza
mchezo wa nusu fainali dhidi ya Lyon utakaopigwa nchini
Ureno.


Tayari PSG ishajikatia tiketi ya kushiriki fainali baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Leipzing usiku wa
kuamkia leo.


Fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 23, Uwanja wa Estadio do
Sport Lisbon.
Pete Jenson, mwandishi wa Daily Mail amesema kuwa kuna
mpasuko mkubwa wa nafsi za nyota wengi ndani ya Klabu ya
Barcelona jambo linalowafanya wengi wafikirie kuondoka.


Mbali na Suarez pia staa wao namba moja ambaye alitupia
jumla ya mabao 25 ndani ya La Liga, Lionel Messi naye
anatajwa kupiga hesabu za kutimka ndani ya kikosi hicho.

Exit mobile version