Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu, limesema ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen, bado unaendelea bila ya kudhibitiwa.
Shirika hilo limetaja idadi ya watu walioathirika na Kipindupindu nchini Yemen kuwa zaidi ya laki tatu, na kuongeza kwamba vita , umasikini na kuporomoka kwa miundo mbinu, kuwa sababu kubwa ya mripuko wa ugonjwa huo unaouwa , kutokana na chakula na maji.
Miaka miwili ya vita kati ya serikali ya Rais Abd-Rabbu Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Kishia wa jamii ya Houthi,vimeivuruga sekta ya afya nchini humo na kusababisha maelfu ya watu kuambukizwa kipindupindu.
