Kiungo wa Simba aingizwa mjini.

Kiungo wa Simba Mghana James Kotei, amekaribishwa nchini Tanzania kwa kulizwa na wezi wa mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam, kwa kuibiwa simu yake ya mkononi.

 

Kiungo huyo akiwa maeneo ya mitaa ya Msimbazi alijikuta akiingia mikononi mwa vibaka waliobobea kwa wizi, na kumuibia simu ya mkononi yenye thamani ya Sh milioni 1.4.

Simu hiyo alipewa zawadi na mmoja wa wanachama wa Simba, siku chache kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii iliyoikutanisha Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Maelezo kutoka kwa mtu wa karibu wa klabu hiyo amedai kuwa, mchezaji huyo alistuka baada ya kufika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Msimbazi akitokea Hotelini alikofikia na kujikuta hana simu.

Alipoulizwa Kotei kuhusiana na suala hilo amekiri wazi kuwa ni kweli amepatwa na balaa hilo, na kudai kuwa amepoteza mawasiliano yake muhimu.

 

Exit mobile version