Kongamano la kwanza la Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu afya barani Afrika limemalizika jana

In Kimataifa

Kongamano la kwanza la Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu afya barani Afrika limemalizika jana mjini Kigali, Rwanda, kwa kutoa ahadi ya kutimiza upatikanaji wa huduma za afya kwa wote barani humo.

Kongamano hilo la siku mbili lilikutanisha wajumbe zaidi ya 700 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wasomi, mawaziri wa afya, mashirika ya kiserikali na ya kijamii, na sekta binafsi.

Wajumbe hao walijadili masuala muhimu ikiwemo kutumia kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wote kama njia kuu ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya, ambayo yanahakikisha maisha bora na kuinua afya ya watu wote katika umri wote, na kuimarisha na kudumisha maendeleo ya nguvukazi kwenye sekta ya afya.

Wajumbe hao pia wametoa wito kwa serikali barani Afrika kuongoza na kusimamia vitendo vinavyolenga kujenga majukwaa ya uratibu na mfumo wa kanuni ili kutimiza upatikanaji wa huduma za afya, kuongeza uwekezaji wa ndani, na kusimamia na kutoa ripoti za maendeleo yanayopatikana.

 

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu