Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani

In Kimataifa

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani.

Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.

Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.

Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .

 

Kitengo cha habari cha taifa hilo KCNA kilisema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53.

Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu na pwani yake ya kaskazini , kulingana na maafisa wa Japan.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo

KCNA imeongezea kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye alishuhudia kufyatuliwa kwa kombora hilo alitangaza ‘kwa majivuno’ kwamba sasa tumekamilisha lengo letu la miaka mingi la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.

Ripoti hiyo imesema kuwa kama taifa lenye nguvu za kinyuklia na linalopenda amani, Korea Kaskazini itafanya kila iwezalo kutekeleza lengo lake la kuleta amani na udhabiti duniani.

Imesema kuwa, silaha zake za ulinzi dhidi ya sera ya kibepari ya Marekani, hazitatishia taifa lolote duniani iwapo maslahi ya Korea Kaskazini hayatakiukwa.”Hilo ndio tangazo letu”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu