Korea Kaskazini imeonya kuwa itasababisha maumivu na mateso makubwa kwa Marekani, ambayo hayajawahi kushuhudiwa.
Imetoa angalizo hilo kama utawala wa mjini Washington, utaendelea kushinikiza Korea Kaskazini iwekewe vikwazo vikali zaidi, kwa kufanya jaribio la sita la silaha za nyuklia.
Marekani inataka Korea Kaskazini iwekewe vikwazo vya kutouziwa mafuta, mali za kiongozi wa taifa hilo zizuiwe, uuzaji wa nguo katika nchi za nje ukomeshwe, na malipo ya wafanyakazi wageni raia wa Korea Kaskazini yasitishwe.
Marekani inataka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kupiga kura leo kuridhia vikwazo hivyo licha ya upinzani kutoka kwa China na Urusi.
