Korea Kaskazini inaaminiwa imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi ya kutoka ardhini kwenda baharini katika pwani yake ya mashariki kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini.
Urushaji huo wa makombora umekuja siku moja baada ya Korea Kusini kuahirisha kuanzisha utaratibu wa mfumo wa Marekani wenye utata wa kupambana na makombora, ulioundwa kuzuia mashambulizi ya Korea Kaskazini.
Hilo ni jaribio la nne la makombora lililofanywa na Korea Kaskazini tokea rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae kukamata madaraka Mei 10 na kuahidi kufanya mazungumzo na Korea kaskazini.
Rais huyo wa Korea Kusini amesema shinikizo na vikwazo vya kiuchumi pekee vimeshindwa kutatua kitisho kinachoendelea cha Korea Kusini.
