Korea Kaskazini kuzamisha meli yakubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea.

 

Korea Kaskazini iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishwa  kwa shambulizi moja.

Kundi la meli za Marekani zikiongozwa na Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.

Meli hizo zilitumwa na Rais Donald Trump baada ya onyo kuhusu uvumilivu kumalizika dhidi ya mpango ya nuklia ya Korea Kasakazini

Exit mobile version