Kundi la Tisa lahama Ngorongoro kwenda Msomera.

In Kitaifa

Kundi la 9 la wakazi wenyeji wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro
limeondoka leo Septemba 15/2022 kuelekea kijiji cha Msomera
na kufanya idadi ya kaya zilizohama eneo hilo kufikia 223 zenye
Watu 1233 na Mifugo 7442 

Msisitizo umeedelea kuwekwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT
kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba katika kijiji cha Msomera,
ili iweze kuendana na kasi ya wanao jiandikisha.
Akitoa taarifa ya Maendeleo ya zoezi hilo kwa msemaji mkuu
wa serikali Gerson Msigwa,naibu kamishna wa uhifadhi NCAA
Dkt Christopher Timbuka,amesema kwa sasa idadi ya wanao
jitokeza kujiandikisha kwa hiari imekuwa maradufu na kuanza
kutishia upatikanaji wa nyumba kule Msomera. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond
Mangwala,amesema zoezi hilo linafuata taratibu zote kama
ilivyoelekezwa na serikali,na pia kwa sasa hali ya uhifadhi wa
mimea na wanyamapori katika maeneo waliyohama wananchi
imeanza kurejea kwa kasi na kualika wageni mbali mbali kufika
kujionea uzuri wa Ngoronoro.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mkuu mpya wa chuo cha Arusha asimikwa.

Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuohicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuonihapo.  Mkuu aliyeachia nafasi

Read More...

Naibu Waziri Silinde atoa maagizo mazito Musoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Silindeamemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma VijijiniMkoa wa Mara, Msongela Palela

Read More...

Waziri mkuu abaini madudu ya ajabu mkuranga.

Waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa,janaalifanya mkutano maalaum katika Wilya ya Mkuranga ambapoamebaini mambo kadhaa,likiwemo la watumishi wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu