Kuongezeka kwa ajali nyingi kazini,sekta ya viwanda imekua ikisababisha hasara zitokanazo na fidia pindi mtu anapopata ajali kazini.

In Kitaifa

SEKTA ya viwanda Nchini imekuwa ikisababisha hasara zitokanazo na fidia pindi mtu anapopata ajali kazini, kufuatia sekta hiyo kuongoza kwa ajali nyingi mahala pa kazi.

Katika maeneo mbalimbali ya kazi hapa nchini kumekuwa kukitokea matukio ya ajali, na kusabisha majeruhi na pengine vifo kutokana na kutozingatiwa kwa usalama ama kinga kwa wafanyakazi hali inayosababisha ajali sekta vya viwanda kutajwa, kuongoza katika ajali hizo ambazo zinaweza kuepukika .

Kauli hiyo imetolewa  mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira  Vijana na walemavu ANTHON MAVUNDE wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya afya na usalama mahala pa kazi.

Amesema kuwa sekta ya viwanda kwa maana ya uzalishaji imekuwa ikiongoza kusababisha hasara kwa serikali, na wafanyakazi wake na kuwa katika kipindi cha mwaka 2013 hadi machi mwaka huu kwa Wilaya ya Kinondoni na Ilala ,katika mkoa wa Dar es salaam jumla ya ajali 1153 ziliripotiwa kwa ajili ya kulipwa fidia.

Amesema kuwa katika ajali hizo sekta ya viwanda inaongoza huku ajali hizo zikisababisha hasara ya jumla ya sh. mil 256  zilitumika kulipa fidia kwa wahanga hao ambapo hapa anaeleza baadhi ya hasara zinazosababishwa na ajali hizo.

Kila ifikapo April 28 kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya afaya na usalama mahali pa kazi ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro yakiwa na kauli mbiu ya ‘ongeza wigo wa ukusanyaji  na utumiaji wa takwimu za usalama na afya kuchangia lengo no. 8 la millennia linalosema kazi za staha na ukuaji wa uchumi’.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu