Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela, jana amewaongoza watanzania katika maadhimisho ya kumbukumbu ya ajali ya Meli ya Mv. Bukoba, iliyotokea Mei 21 mwaka 1996 kilometa chache kabla ya kufika Bandari ya Mwanza ikitokea mkoani Kagera.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la kata ya Igoma wilayani Nyamagana yaliko makaburi ya marehemu wa ajali hiyo.
Kumbukumbu hii imetanguliwa na ibada maalum kutoka kwa viongozi wa kidini, waliogusia masuala mbalimbali yanayowakumbusha wanadamu kumcha mwenyezi Mungu, kwa kuwa hakuna aliyeiona kesho kuhusu safari ya maisha yake.
