Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambayo haina shule ya kidato cha tano na sita, kwa mara ya kwanza shule ya sekondari ya Emboreet itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani amesema wamejipanga shule hiyo ianze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano, Julai mwaka huu.
Chaula amesema hadi hivi sasa shule ya sekondari Emboreet ya kidato cha nne, imeboreshwa kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano, kwani awali wilaya ilikuwa haina shule ya kidato cha tano na sita.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipiti eck, mkurugenzi mtendaji Yefred Myenzi na madiwani, wametenga sh 12 milioni, kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya shule hiyo.
Amesema diwani wa kata ya Emboreet, Christopher Kuya anastahili kupongezwa, kwa kusimamia kitendo cha shule hiyo kufanikiwa kuwa na hatua ya kidato cha tano na sita kwani ni maendeleo kwa Simanjiro
