Lazaro nyalandu ajivua ubunge ahama ccm

Mbunge wa chama cha Mapinduzi CCM Lazaro Nyalandu, amejiuzulu wadhifa wake, na kusema kwamba anataka kuhamia chama cha upinzani Chadema.
Bw Nyalandu aliyewahi kuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano, amesema amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama cha mapinduzi ikiwemo ubunge.

Nyalandu amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na muenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu.
Antena imeinasa sehemu ya maelezo ya mheshimiwa Nyalandu, alipokuwa akitangaza uamuzi huo huku akikitaka chama cha Demokrasia na maendeo CHADEMA kumpokea kama wakiona inafaa.

TIZAMA VIDEO

Exit mobile version