LHRC champongeza Magufuli.

In Kitaifa
Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii Nguza Viking.
 
Pamoja na pongezi hizo LHRC, imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo..
“Tunampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 61 kati ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia ukurasa wao wa Twiiter.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
LHRC imeongeza, “Tunamsihi Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta sheria zinazoruhusu uwepo wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya kifungo cha maisha kuwa adhabu mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44 gerezani

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu