Kituo cha sheria na haki za Binadamu pamoja na mashirika ya utetezi wa haki za binadamu, wamekutana na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa tamko lao kuhusu hali ya usalama nchini.
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Bi Bisimba amesema kuwa, matukio mabaya yanazidi kushamiri na kuitaka serikali kutafuta ufumbuzi wa hilo.
Baada ya kusema hayo Bi Bisimba ametaka kuundwe kwa tume huru ya uchunguzi yakinifu, itakayoundwa na Bunge ili kuweza kuwapata wahusika wa matukio mbalimbali, yakiwemo Tundu Lisu, Nape Nnauye na wengineo ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo husika.
