Licha ya Tanzania kukadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 45, lakini watu wengi hawajawa na mwamko wa kuandika wosia.
Hayo yameelezwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson jijini Dar es salaam.
Emmy amesema kuwa kwa miaka 10 iliyopita, watu waliojitokeza kuandika wosia ni mia 4 na 38, huku waliochukua hosia zao wakiwa 22 pekee.
Emmy amezitaja takwimu za mwaka huu kuanzia Januari hadi Mei kuwa, wosia zilizoandikwa ni 37 pekee
