Manchester city wameshinda michezo 15 mfululizo kwenye mashindano yote msimu huu, wakiongoza ligi ya Uingereza kwa alama nane.
City walikwea zaidi kileleni baada ya kuichapa Arsenal 3 – 1 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ethiad siku ya Jumapili kabla ya Manchester United kupoteza dhidi ya Chelsea, City kwa sasa ni kama hawazuiliki
Alan Shearer anaamini kinachozinyima usingizi timu nyingine kwenye mbio hizo za ubingwa ni namna ambavyo City wameimarika toka walipomaliza msimu uliopita wakiwa nyuma ya mabingwa Chelsea kwa alama 15 kwenye msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola kukinoa kikosi hicho.
City wanazidi kusonga mbele wakiwa na magoli 38 kutoka kwa michezo 11 ambayo wameshacheza msimu huu wanonekana kuimarika sana katika safu ya ushambuliaji na ulinzi.
Katika mchezo na washika mitutu wa London golikipa Ederson aliokoa mkwaju wa Aaron Ramsey ambao ulikuwa unatokomea kimiani, wachambuzi wanasema msimu uliopita wakiwa na golikipa Claudio Bravo bila shaka mkwaju huo ungekuwa goli
Na kama ungetinga wavuni ingekuwa 1-1 badala ya 1-0 na matokeo hayo yangeweza kabisa kubadili hali ya mchezo
Inaonekana Pep Guardiola amejifunza kutokana na makosa waliyoyafanya msimu ulipita kiasi cha kuwa tishio kwa vilabu vingine msimu huu
Alan Shearer anasema ailipokuwa Blackburn, Manchester United walikuwa wakiongoza kwa alama 12 baaada ya michezo 16 ya msimu wa 1993 – 94 lakini walilipambana na kuwafikia kufikia mwezi Aprili.
