Ligi ya mabingwa Ulaya kutimua vumbi.

 

Ligi ya Mabingwa Ulaya imerejea msimu wa 2017/18, huku vigogo wote wakishuka uwanjani leo na kesho.

Beki wa PSG Thiago Silva ameenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, presha ni kubwa kikosini kwao kutokana na usajili uliofanyika.

Silva anasema ujio wa Neymar na Kylian Mbappe, utawafanya wawe na presha kubwa kwa kuwa watu wengi watahitaji mambo makubwa kutoka kwenye timu yao, ambao inatarajiwa kukipiga dhidi ya Celtic katika michuano hiyo.

Ratiba ya game za leo ambazo zitapigwa kuanzia saa 3:45 Usiku ni Celtic vs PSG,Benfica vs  CSKA, Man U vs Basel
Olympiakos vs Sporting,Bayern München vs Anderlecht,Chelsea       vs Qarabağ,Roma vs Atlético Madrid, Barcelona vs Juventus
PSG ipo nchini Scotland kwa ajili ya mchezo huo, ambapo wababe hao wa Ufaransa watakuwa na nia moja tu ya kupata ushindi, kwa kuwa mastaa waliosajiliwa ni wagharama kubwa.

Exit mobile version