Ligi ya Ujerumani kuanza leo

In Kimataifa, Michezo

Ligi ya Ujerumani-Bundesliga inaanza tena leo, na kuifanya kuwa ligi kubwa ya kwanza barani Ulaya ambayo ilisitishwa, ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kukabiliana na janga la corona. Asasi yenye dhamana na ligi hiyo DFL, ilimshawishi Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na viongozi wa majimbo kuruhusu kufanyika kwa mchuano huo, kwa makubaliano ya kufanya jitihada za hali ya juu za kudhibiti maambukizi. Kabumbu itasakatwa viwanja vikiwa vitupu. Ujerumani ikabiliwa na janga la corona huku ikiwa na vifo vichache, ikilinganisha na mataifa mengine ya ulaya lakini suala la mikusanyiko bado ni la hatari. Miongoni mwa mechi zitakazovuta wengi ni Borussia Dortmund na Schalke 04. Kwa kawaida mchuano huko unavutia umma watu 82,000 uwanjani lakini safari hii uwanja utakuwa mtupu. Jumapili Bayern Munich itafuana na Union Berlin.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu