Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)na Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Tundu Lissu ameshambuliwa na risasi mchana huu.
Mbunge huyo kwa sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoani Dodoma
Mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea wakati mbunge huyo akiwa nyumbani kwake.
Chama hicho kimelaani vikali tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi , Jires Mroto amesema wameanza uchunguzi wa tukio hilo.
“Tunaomba wananchi wenye taarifa ya uhalifu huu, waweze kujitokeza” amesema Kamanda Mroto.
Taarifa zaidi zitakuijia.
