Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Isaac Joseph amewataka wanawake wajasiria mali jamii ya wafugaji kutoka nchini Kenya kuja nchini tanznia haswa katika wilaya hiyo ya monduli kwa ajili ya kujenga ushirikiano wa pamoja na kuwekeza katika viwanda.
Akizungumza na wanawake hao wabunge,na makatibu tarafa kutoka nchini Kenya ,mara baada ya kufanya ziara ya kumtembelea waziri mkuu staafu Edward lowasa amesema amefurahishwa na ziara hiyo kwa kuwa wanawake hao kwa kiasi kikubwa wanepiga hatua kubwa za maendeleo.
Amesema hapo mwanzo jamii ya wafugaji haswa mtoto wa kike ilikuwa nyuma kimaendeleo ,na hata kielimu hivyo ni jambo la kutia moyo kwa wanawake hao kuweza kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuwekeza katika sekta mbali mbali.
Mbunge wa kaunti ya kajiado Charles lekatoo amesema kuwa ni vyema jamii ikabadilika na kutoa fursa kwa watu wote bila kujali jinsia kwa kuwa uwezo wa mtu hautegemei jinsia.
